Kivinjari kinachokupa kipaumbele

Zuia matangazo. Okoa data. Na upate kurasawavuti zenye kasi. Kwa kubadilisha kivinjari chako tu.

Utafutaji wa faragha

Matokeo bora, majibu ya AI na bila rekodi ukitumia Brave Search.

Mratibu wa AI uliojengwa ndani

Pata majibu, unda maudhui na zaidi. Katika kivinjari.

Leo AI

VPN yenye nguvu zaidi

Linda kila programu, kwenye kifaa chako chote.

Ngome + VPN

Je, Wavuti wa kwanza wa mtumiaji unafanana vipi?

Faragha bora. Kurasa wavuti za kasi. Usogezaji rahisi. Na hali zinazowajali watu zaidi ya faida ya kampuni ya teknolojia.

Wavuti, bila usumbufu

Brave huzuia matangazo mengine kwenye kila wavuti. Yaani matangazo ya video, matangazo ya utafutaji, matangazo ya mitandao ya jamii na zaidi.

Na ibukiz za “Kubai vidakuzi?” zinazoudhi? Ndiyo, tunazizuia pia.

Okoa data, okoa betri, okoa muda.

Bila taka isiyohitajika, unaokoa data ya Wi-Fi na data ya kifaa cha mkononi, muda wa betri na CPU. Na tovuti zinapakia 3x-6x haraka zaidi. Kusubiri muda mfupi = unapata muda zaidi kwenye siku yako.

Faragha ya kipekee

Ngao dhidi ya kufuatilia na kuchukua taarifa za utambilisho. VPN ya kulipia ambayo inaweza kusimba kwa njia fiche kila muunganisho bila kujali ulipo. Kwa chaguomsingi Kidhibiti cha Faragha cha Kimataifa ili kusimamisha tovuti kuuza na kushiriki data yako.

Yote haya (na zaidi) katika kifurushi kimoja rahisi zaidi.

Usalama uliojengewa ndani, kwa chaguomsingi

Brave inajitahidi zaidi. Hakuna kubonyeza, hakuna viendelezi, hakuna PhD inayohitajika.

Kubadilisha ni rahisi

Wavuti wa kasi, faragha zaidi, wenye usumbufu kidogo upo umbali wa sekunde 60 tu.

Pakua tu Brave, leta vipendwa kutoka kwenye kivinjari chako cha zamani na… Umekamilisha!

Wavuti ulio na matangazo machache

Angalia baadhi ya tovuti maarufu katika Brave dhidi ya vivinjari vingine. Umeona tofauti?

Chukua slaida ili uone tofauti baina ya Brave na vivinjari vingine

brave
chrome
brave
chrome
brave
edge
brave
edge
brave
firefox
brave
firefox
brave
safari
brave
safari

Kushinda kwa faragha, utendaji na vipengele

Angalia jinsi Brave inavyotopea dhidi ya vivinjari vingine kwa ulinganishaji huu wa kina.

Brave dhidi ya Chrome

Kuhusu faragha na utendaji, Chrome iko nyuma sana ya Brave.

Angalia jinsi Chrome inavyolinganishwa

Brave dhidi ya Firefox

Kwa kuwahi kutumiwa sana, Firefox imeshuka hadi nafasi ya katikati kama njia mbadala ya Big Tech.

Angalia jinsi Fireforx inavyolinganishwa

Tafuta na Brave dhidi ya Google

Programu maarufu sana ya utafutaji inatumia data nyingi ya watumiaji, ikiweke kipaumbele kwenye matangazo badala ya majibu.

Angalia jinsi Google inavyolinganishwa

Tafuta na Brave dhidi ya DuckDuckGo

Injini ya utafutaji "mbadala" inayoendeshwa na Microsoft Bing.

Angalia jinsi DDG inavyolinganishwa

Kivinjari kinachookoa muda wako, si taarifa binafsi zako

Pakua Brave for Android, iOS, Linux, macOS, au Windows

App Illustration
*Brave husaidia uwekaji wa sera ya makundi ya biashara ili kugeuza kukufaa vipengele vinavyowashwa/kuzimwa kwa ajili ya shirika lako.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, Kivinjari cha Brave ni salama?

Brave ni moja ya vivinjari salama zaidi kwenye soko leo. Huzuia matangazo na vifuatiliaji vinavyovamia faragha. Huzuia hifadhi ya data ya mhusika mwingine. Hulinda dhidi ya ukusanyaji data ya kivinjari. Hubadilisha kila ukurasa wavuti iwezekanavyo ili kulinda miunganisho ya https. Na hufanya yote haya kwa chaguomsingi.

Pia hujenga programu huria ya Wavuti wa Chromium, inayowezesha vivinjari vinavyotumiwa na mabilioni ya watu kote duniani. Msimbo huu wa chanzo unakaguliwa na watafiti zaidi wa usalama kuliko kivinjari kingine chochote. Yaani, Brave si salama tu, bali pia ni salama zaidi kuliko kivinjari kingine chochote. Pata maelezo zaidi.

Je, ninapaswa kupakua na kusakinisha Brave vipi?

Brave inapatikana kwenye takribani kompyuta zote za mezani (Windows, macOS, Linux) na takribani kila kifaa cha mkononi (Android na iOS). Ili kuanza, pakua tu kivinjari cha Brave cha kompyuta ya mezani, cha Android, au cha iOS.

Je, Brave ina VPN?

Ndio! Brave Firewall + VPN hulinda kila kitu unachofanya mtandaoni, kwenye kifaa chako kizima, hata nje ya Kivinjari cha Brave. Usajili mmoja unasimamia hadi vifaa 5, kwenye Android, iOS, na kompyuta ya mezani.

Je, Brave inazuia matangazo ya YouTube?

Ndiyo, kivinjari cha Brave kinaweza kuyazuia matangazo kwenye tovuti za video kama YouTube. Hiyo ni pamoja na matangazo kwenye ukurasa, matangazo ya mwanzo na katikati ya video, matangazo ya mwisho wa video na zaidi. Kwa kuzuia matangazo, unapata hali bora ya utumiaji isiyo ya usumbufu na upakiaji haraka wa video. Pata maelezo zaidi kuhusu uzuiaji wa matangazo ya YouTube ya Brave.

Je, injini ya Tafuta na Brave ni nini?

Tafuta na Brave ni injini ya utafutaji ya faragha na huru ambayo ni chaguomsingi kwa watumiaji wapya wengi wa kivinjari cha Brave. Pia inapatikana katika kivinjari kingine chochote kwenye search.brave.com. Tafuta na Brave inatoa matokeo ya haraka na sahihi kutoka kwenye takwimu yake huru ya Wavuti na ina vipengele vya kipekee kama vile injini madhubuti ya majibu ya AI. Kinyume cha injini nyingine za utafutaji, Tafuta na Brave haikurekodi; haiwezi kushiriki, kuuza wala kupoteza data binafsi yako, kwa sababu haikusanywi. Pata maelezo zaidi kuhusu Tafuta na Brave.

Je, ni lugha gani zinazopatikana katika Brave?

Tafuta na Brave inapatikana katika takribani lugha 160, ikiwa ni pamoja na lahaja nne tofauti za Kichina. Tafuta na Brave inapatikana kwa sasa katika karibu lugha 20 tofauti, huku msaada kwa hata lugha zaidi ukiwa njiani.

Je, ni nani anayemiliki Brave?

Kivinjari cha Brave, Tafuta na Brave na vipengele vyao vyote mbalimbali vimetengenezwa na Brave Software Inc, kampuni huru ya binafsi. Brave haiwajibikii kampuni nyingine yoyote ya teknolojia na inajitahidi kila siku kupambana na matumizi mabaya ya faragha ya Big Tech. Brave ipo ili kuwasaidia watu halisi, si kampuni ya teknolojia isiyoonekana.

Je, Brave ni programu huria?

Ndio. Kivinjari cha Brave kimejengwa kwenye programu huria ya Chromium Web na msimbo wetu wa seva-teja unatolewa kwa mujibu wa Mozilla Public License 2.0.

Je, Brave inalinganishwaje na Chrome?

Kwa lugha rahisi, Kivinjari cha Brave kina kasi mara 3 zaidi ya Google Chrome. Kwa kuzuia mtangazo na vifuatiliaji vinavyohitilafiana na faragha kwa chaguomsingi, hakuna vitu vingi vya kupakia kila ukurasa wavuti unaotembelea. Hiyo ina maana kuwa kurasa zinapakiwa haraka zaidi na hivyo kuokoa muda, pesa na muda wa kudumu wa betri. Pia inamaanisha kwamba unapata huduma ya kasi mtandaoni. Pata maelezo zaidi.

Je, Brave ni ya bila malipo?

Ndiyo, Brave ni ya bila malipo unapoitumia. Pakua tu kivinjari cha Brave kwa kompyuta ya mezani, kwa Android, au kwa iOS ili uanze. Pia unaweza kutumia Tafuta na Brave bila malipo kutoka kwenye kivinjari chochote katika search.brave.com, au iweke kuwa injini yako ya utafutaji chaguomsingi.

Brave pia ina baadhi ya vipengele bora vya usajili, ikiwa ni pamoja na Brave Talk Premium na Brave Firewall + VPN.

Je, BAT ni nini na ninaweza kuijuaje?

BAT ni ufupisho wa Basic Attention Token. BAT ni mali ya dijitali na sehemu muhimu (lakini ya hiari kabisa) ya mfumo wa mazingira wa Brave Rewards. Hii hapa jinsi inavyofanya kazi:

Brave Rewards inakupa chaguo la kutazama matangazo ya kulinda faragha ya mhusika mwingine huku ukivinjari (matangazo haya yanatoka kwenye mtandao wa Brave Private Ads). Ukichagua kuyatazama, unapata BAT kupitia programu ya Brave Rewards.

Unaweza kuweka BAT kama mali mengine yoyote ya dijitali, au kuitumia kuwapa bahshishi wachapishaji wa maudhui unayopenda. Brave hata inakupa njia salama ya kuhifadhi BAT (na mali mengine yoyote), ukitumia Brave Wallet. Na, tena, Brave Rewards ni programu ya hiari kabisa.

Kampuni nyingine za teknolojia huiba data yako ili kuuza matangazo—kwazo, wewe ni bidhaa. Brave ni tofauti. Tunadhani kwamba umakini wako ni muhimu (na wa faragha), na kuwa unapaswa kupata mgao sawa wa mapato kwa tangazo lolote unalochagua kutazama. Mgao huo sawa unazawidiwa katika BAT.