Msingi Ramani wa BAT 3.0: Kuzingatia Ukuaji wa Kwenye Mnyororo

Msingi Ramani wa BAT 3.0: Kuzingatia Ukuaji wa Kwenye Mnyororo. Katika mfumo wa zawadi za Brave na watengeneza maudhui wa Brave, mpango huu unalenga kuondoa mawakala wa kati kwenye mtiririko wa BAT kupitia jukwaa, kupanua chaguzi za usimamizi binafsi wa malipo na michango, na kutoa njia mpya kwa watumiaji kupata na kutumia BAT. Nje ya Brave, msisitizo wetu utakuwa kukuza ukuaji wa BAT na kupanuka ndani ya uchumi mpana wa umakini, kwenye viambajengo (Blockchains) zote zinazoweza kuunga mkono BAT. Hii inamaanisha kutoa fursa zaidi kwa miradi, programu gatuzi (dApps), na waandishi wa maudhui kuingiza kazi zao kwenye mfumo wa matumizi wa BAT na kukua pamoja na watumiaji wa Brave na BAT.

Ramani bora ya maendeleo hutoa mwelekeo wa pamoja na jumla lakini hubakia kuwa rahisi ili kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa. Tunapojaribu na kupata mafanikio ya soko, baadhi ya vipengele vya Msingi Ramani vinaweza kupunguzwa kutiwa msisitizo huku vingine vikipewa kipaumbele zaidi.

BAT katika zawadi za Brave

Kwa kuzingatia msingi ramani wa BAT 3.0, tunatarajia kuzindua Zawadi za Brave 3.0 katika robo ya kwanza ya 2025, ikiwa ni maboresho ya hali ya juu kwa zawadi za Brave.

Katika zawadi za Brave 3.0, tunalenga kujumuisha:

Njia mpya za kupata zawadi

  1. Bahati nasibu ambapo watumiaji wanaweza kupokea kiasi kikubwa cha BAT, vizidisho vya mapato, na bonasi nyingine
  2. Zawadi kwa kukamilisha majaribio ya kwenye mnyororo
  3. Zawadi kwa kukamilisha tafiti

Chaguzi mpya za usimamizi binafsi

Kupanua chaguzi za malipo kwa usimamizi binafsi ili kusaidia viambajengo (blockchains) mbalimbali na mitandao ya safu za 2.0.

Muundo mpya na mabadiliko ya UX 

Zawadi 3.0 itajumuisha muundo mpya kabisa na uzoefu bora wa mtumiaji. Muundo huu mpya unatumia mfumo wa kimoduli, kurahisisha:

  1. Kuonyesha matumizi ya BAT (programu gatuzi (dApps), ununuzi, nk.)
  2. Kuunda uzoefu mpya wa matangazo ya Brave na fursa za mapato
  3. Kuunganisha Lipa kwa BAT inapofaa katika UX ya zawadi
  4. Kuboresha ugunduzi wa waunda programu wa Brave na kuunganisha watumiaji na waandishi wa maudhui

Ukuta wa Zawadi za Ofa

  1. Kuanzisha Ukuta wa Ofa mpya na wenye faida za kipekee kwa watumiaji wa zawadi za Brave. Ukuta wa Ofa itajumuisha ofa za papo hapo, zinazolingana na eneo la mtumiaji, na ofa maalumu za washirika.
  2. Kuunganisha mfumo wa matangazo wa Brave kufanya kazi kwa kushirikiana na ukuta wa Ofa (Offer Wall). Kwa mfano, kutumia algoriti za kujifunza mashine za ndani kuonyesha taarifa za ofa zinazofaa au kufunguliwa.

Kuondoa Wawakilishi wa Kati (Disintermediation)

  1. Kuendelea kuendeleza na kuchapisha kazi kwenye Boomerang, itifaki ya motisha ya faragha inayothibitishwa
  2. Kushirikiana na viamba jengo (blockchains) na mifumo ya mikataba mahiri inayoweza kusaidia utekelezaji wa mikataba mahiri ya Boomerang

BAT katika E-commerce

  1. Lipa kwa BAT kwa bidhaa za Brave kama Brave Premium (Brave VPN, Talk, Leo, nk.)
  2. Lipa kwa BAT kwa bidhaa kutoka Brave Merch Store
  3. Kuongeza msaada wa BAT kwenye njia kuu za malipo ya kripto

BAT katika Waumbaji wa Brave

Kupanua majukwaa yanayoungwa mkono

  1. Kuongeza idadi ya majukwaa ya kijamii kwa waandishi wa maudhui kujiandikisha akaunti zao kwenye Brave Creators, ikiwemo Rumble, Odyssey, na zaidi. Hii itaruhusu waandishi kukusanya BAT na michango mingine ya crypto kwenye viambajengo (blockchains).
  2. Kushirikiana na majukwaa ya Web3 ili kuongeza matumizi ya BAT.

Kupanua msaada wa blockchain na Safu ya 2 (Layer 2) kwa michango

  1. Kuruhusu waandishi kuunganisha anwani za kwenye mnyororo kutoka viambajengo vingi na zaidi na mitandao ya Safu za 2 (Layer 2).
  2. Kuongeza msaada wa majina ya vikoa vya Mtandao wa 3 (Web3).

Michango ya kwenye mnyororo

Allowing users to make recurring donations to Brave content writers via on-chain channels.

Programu za Ukuaji wa watengeneza Maudhui wa Brave

Mpango huu utatumia mfumo wa Matangazo ya Brave kukuza hadhira na mapato ya waandishi kupitia ushirikiano na jumuiya ya Brave & BAT. Itawapa waunda maudhui upatikanaji wa kipekee kwa washirika wa Brave, ikijumuisha huduma na zana za kisasa za AI na Web3.

BAT katika AI

Kufanya utafiti na kuendeleza matumizi ya BAT katika AI. Tunapojaribu, tutazingatia majukumu yanayowezekana ya BAT katika Brave Leo na kuunganisha chaguzi za malipo ya premium kwa kripto.

Jumuiya ya BAT?

Programu ya mabalozi wa BAT

  1. Kuzindua mpango wa rufaa wa Brave Ads Self-Serve kwa mabalozi wa BAT.
  2. Kukuza upokeaji wa BAT kwenye viambajengo vyingi kupitia warsha zinazoongozwa na mabalozi. 
  3. Endesha matumizi ya BAT katika maeneo mapya kupitia utafsiri wa maudhui na mipango inayohusiana na tamanduni, inayoongozwa na mabalozi wa kienyeji.

Ushirikiano

  1. Kushirikiana na majukwaa ya Web3 ili kuongeza matumizi ya BAT.
  2. Kufanya ushirikiano na KOLs kwa kampeni maalum za BAT.
  3. Kuandaa matukio ya kipekee kwa wamiliki wa BAT.

Programu

  1. BAT x Adam Ape NFT Program: Kuchunguza mpango wa matumizi kwa wamiliki wa NFT. Mifano inayowezekana ni upatikanaji wa kipekee wa punguzo kwenye bidhaa za Brave premium na bidhaa za BAT/Brave n.k.
  2. Kuendeleza tafsiri na mafunzo ya maudhui ya elimu ya BAT katika lugha za kienyenji.

Maudhui na Ushirikiano

  1. Kupanua ufikiaji wa ECHO NFT Magazine kupitia ushirikiano na waandishi wa maudhui.
  2. Kuonyesha hadithi za mafanikio za Waunda Maudhui wa Brave.

Shirikiana Nasi

Ikiwa mradi wako wa Web3/kripto, Programu gatuzi (dApp), kiambajengo (blockchain), au mtandao wa Web3 unalingana na malengo ya msingi ramani wa BAT 3.0 na ungependa kushirikiana na Brave na Basic Attention Token, wasiliana nasi kupitia bizdev@brave.com.

Ready for a better Internet?

Brave’s easy-to-use browser blocks ads by default, making the Web faster, safer, and less cluttered for people all over the world.